Kutokana na utafiti uliofanywa na HakiElimu hivi karibuni na kuzinduliwa rasmi leo, HakiElimu imependekeza Kamati ya Uidhinishaji wa Vitabu vya Kiada (EMAC) ifanyiwe maboresho ili kulinisuru taifa dhidi ya jamii ya wasomi bandia.
Mapendekezo hayo yametokana na ukweli kwamba vitabu vingi vya kiada ambavyo vimepitishwa na kamati hiyo vina makosa ambayo yanawapotosha walimu na wanafunzi.
Mapendekezo hayo yametokana na utafiti uliofanywa na HakiElimu (2011) kutathmini ubora wa vitabu vya hisabati vya shule za msingi na kubaini kuwa na makosa mengi kwenye vitabu ambavyo vimeidhinishwa na EMAC. Mapendekezo hayo yanalenga kuiboresha kamati hiyo muhimu katika utoaji wa elimu nchini.
Hayo yalisemwa leo na Mchambuzi wa Sera wa HakiElimu Bwana Mtemi Zombwe wakati akiwasilisha matokeo ya utafiti uliofanywa na HakiElimu kuhusu Uhusiano wa Ubora wa Mitaala na Utoaji Elimu Bora.mikoa iliyoshirikishwa kwenye utafiti ni Arusha,Iringa,Tanga,Mwanza,Tabora na Shinyanga.
"kama EMAC inapitisha vitabu vibovu nchi itakua na wasomi wabovu na hivyo kuwa na wasomi bandia ambao hawataweza kusukuma gurudumu la maendeleo nchini," alisema Mtemi Zombwe ambaye ni mtafiti wa sera katika Idara ya Sera na Utetezi, HakiElimu.
No comments:
Post a Comment