| ||
Mshambuliaji hatari wa timu ya Inter Milan ya Italia, Samuel Eto'o | Mshambuliaji Samuel Eto'o wa timu ya taifa ya Cameroon na timu ya Inter Milan ya Italia atakuwa mchezaji soka anayelipwa pesa nyingi kuliko wachezaji wote duniani akiwafunika Ronaldo na Messi baada ya kukubali kusajiliwa na timu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi ambapo atakuwa akilipwa zaidi ya Th. Milioni 600 kila wiki. | |
Mshambuliaji hatari wa timu ya Inter Milan ya Italia, Samuel Eto'o anatarajiwa kumwaga wino kusajiliwa na timu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi. Usajili huo utamfanya Eto'o apokee mshiko wa nguvu wa kiasi cha paundi milioni 20 kwa mwaka ambapo kila wiki atakuwa akilipwa paundi laki tatu ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 600. Eto'o ambaye sasa ana umri wa miaka 30, anatarajiwa kuingia mkataba wa miaka mitatu na klabu hiyo tajiri ya Urusi inayomilikiwa na bilionea wa biashara ya mafuta, Suleiman Kerimov. Usajili huo uko kwenye hatua za mwisho ambapo Inter Milan inaitaka klabu ya Anzhi itoe kitita cha paundi milioni 30 ili iweze kumnunua mchezaji huyo. Eto'o atakuwa mchezaji tajiri kuliko wote duniani akiwapiku Cristiano Ronaldo wa Real Madrid anayelipwa paundi milioni 12 kwa mwaka na Lionel Messi wa Barcelona anayelipwa paundi milioni 10.5. Klabu ya Anzhi katika kujiimarisha zaidi imemsajili pia beki mkongwe wa Brazil, Roberto Carlos ambaye sasa ana umri wa miaka 38. |
Friday, August 19, 2011
Eto'o Kuwa Mchezaji Tajiri Kuliko Wote Duniani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment