Pages

Friday, August 19, 2011

Eto'o Kuwa Mchezaji Tajiri Kuliko Wote Duniani



NewsImages/5888114.jpg
Mshambuliaji hatari wa timu ya Inter Milan ya Italia, Samuel Eto'o

Mshambuliaji Samuel Eto'o wa timu ya taifa ya Cameroon na timu ya Inter Milan ya Italia atakuwa mchezaji soka anayelipwa pesa nyingi kuliko wachezaji wote duniani akiwafunika Ronaldo na Messi baada ya kukubali kusajiliwa na timu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi ambapo atakuwa akilipwa zaidi ya Th. Milioni 600 kila wiki.
Mshambuliaji hatari wa timu ya Inter Milan ya Italia, Samuel Eto'o anatarajiwa kumwaga wino kusajiliwa na timu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi.

Usajili huo utamfanya Eto'o apokee mshiko wa nguvu wa kiasi cha paundi milioni 20 kwa mwaka ambapo kila wiki atakuwa akilipwa paundi laki tatu ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 600.

Eto'o ambaye sasa ana umri wa miaka 30, anatarajiwa kuingia mkataba wa miaka mitatu na klabu hiyo tajiri ya Urusi inayomilikiwa na bilionea wa biashara ya mafuta, Suleiman Kerimov.

Usajili huo uko kwenye hatua za mwisho ambapo Inter Milan inaitaka klabu ya Anzhi itoe kitita cha paundi milioni 30 ili iweze kumnunua mchezaji huyo.

Eto'o atakuwa mchezaji tajiri kuliko wote duniani akiwapiku Cristiano Ronaldo wa Real Madrid anayelipwa paundi milioni 12 kwa mwaka na Lionel Messi wa Barcelona anayelipwa paundi milioni 10.5.

Klabu ya Anzhi katika kujiimarisha zaidi imemsajili pia beki mkongwe wa Brazil, Roberto Carlos ambaye sasa ana umri wa miaka 38.

Wednesday, August 17, 2011

PANYA KITOWEO MSUMBIJI KATIKA KIJIJI CHA MADAMBA......

MDAU KUWA MAKINI SANA NA ULACHO KAMA IKATOKEA SIKU UMETEMBELEA KIJIJI CHA MADAMBA HUKO MSUMBIJI..


Hii ni safari ya baadhi ya wakazi wa kijiji cha Madamba nchini Msumbiji wakielekea porini si kuwinda wanyama ama kulima hapana hii ni safari inayohusisha kukamata panya ambao hutumika kama kitoweo na wengine wakiuzwa kando ya barabara kuu inayopita kijijini hapo.


Wakati panya huyu ameshaadhibiwa kazi ipo kwa mwingine ambaye anaonesha kila jitihada za kuokoa roho yake.

Amenasa huyu kiulaini kabisa hana ujanja.


Wakati mwingine inabidi kuchimba mashimo katika sehemu ambazo wawindaji huhisi kuwa huenda kukawa na Panya.

Kazi kama imeisha kwa mafanikio hivi maana kila muwindaji anaonekana akiwa na Panya wake.


Wakati mwingine moto hutumika katika kuwapata kirahisi Panya wa kitoweo na biashara.


Hapa sasa Panya wako katika maandalizi kabla ya kuchomwa vizuri kisha kupelekwa sokoni kwaajili ya kuuzwa kwa wanaohitaji kitoweo hicho.


Kitu cha Panya sasa kinachomwa.


Huku Mahindi ya kuchoma huku mishikaki ya Panya.


Biashara nzuri wateja ni wengi kweli kweli.


Mdau huyu akiwa anaikonga roho yake kwa kujipatia Panya kwa senti 30 tu za Msumbiji.


Panya kwa ugali mdau raha iliyoje....


Amini usiamini hawa ndio Panya ambao huku Tanzania tumekuwa tukitumia kila njia kuhakikisha kuwa hawaingii katika nyumba zetu kwa kuhofia uharibifu unaoweza kusababishwa na wanyama hao.






Rosti ya Panya ikiwa jikoni mdau....


Wachuuzi wa Panya wakiwa mapumzikoni baada ya purukushani za hapa na pale kugombea wateja.


Unaweza kujionea hapa mdau panya hao hutungwa katika kijiti wakiwa 6-7 hivi wakiwa wamechomwa vizuri kabisa na humgharimu mteja kiasi cha senti 30 za Msumbiji kuweza kujipatia kitoweo hicho.

Kila muwinda panya mwisho wa siku huambulia kiasi cha dola3 za kimarekani ambazo zinawasaidia kuongeza kipato katika familia zao.

About Rural 2 Urban Skoolz

My photo
Dar es Salaam, Tanzania